Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yatinga Top Four EPL, Yaishusha Man United

Arsenal 7 Wachezaji wa Kikosi cha Arsenal

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Washika Mitutu wa London, Timu ya Arsenal imeibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya wenyeji, Watford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vicarage Road mjini Watford.

Mabao ya Arsenal yamefungwa na Martin Odegaard dakika ya tano, Bukayo Saka dakika ya 30 na Gabriel Martinelli dakika ya 52, wakati ya Watford yamefungwa na Cucho Hernandez dakika ya 11 na Moussa Sissoko dakika ya 87.

Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 48 katika mchezo wa 25 na kupanda nafasi ya nne, wakati Watford inabaki na pointi zake 19 za mechi 27, nafasi ya 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live