Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yataka Mudryk aiwahi Man United

Mudryk.jpeg Mykhailo Mudryk

Sun, 15 Jan 2023 Chanzo: Mwanaapoti

Arswnal imeripotiwa kuwa na uhakika mkubwa wa kumsajili Mykhailo Mudryk ndani ya muda ili awemo uwanjani kwenye mechi dhidi ya Manchester United wikiendi ijayo.

Winga huyo amekuwa akihusishwa na mpango wa kutua England, akiwekwa kwenye namba moja katika orodha ya wakali wanaosakwa na miamba hiyo ya Emirates katika dirisha hili la uhamisho wa Januari.

Arsenal ilishuhudia ofa zake mbili za kuhusu staa huyo wa Shakhtar Donetsk zikikataliwa, kabla ya kwenda na ofa ya tatu ya Pauni 62 milioni pamoja na nyongeza nyingine - ambayo kwa sasa inajadiliwa.

Hata hivyo, Shakhtar wanataka mkwanja mrefu na hapo wanaifanya Arsenal kufikiria kuvunja benki wakitumia Pauni 84 milioni ili kumpata mchezaji wao wanayemsaka.

Mudryk yupo zake Uturuki kwenye kambi ya wachezaji wenzake wakienda kufanya mazoezi katika mazingira yenye hali ya hewa ya joto wakati huu ligi yao ikiwa imesimama kupisha kipindi cha baridi.

Kinachoripotiwa ni kwamba Mudryk na wasimamizi wake wameshakubali dili la miaka mitano kikosi cha Arsenal. Na mwenyewe alionekana kuvunja ukimya akiweka wazi kuhusu mpango wa kwenda kuvaa jezi za The Gunners.

Arsenal leo Jumapili watashuka uwanjani kukipiga na Tottenham Hotspur kwenye North London derby, kabla ya wikiendi ijayo kukabiliana na vigogo wengine wa Big Six, Man United.

Chanzo: Mwanaapoti