Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yapewa akili ya ubingwa

Sfsf Arsenal yapewa akili ya ubingwa

Fri, 30 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Petit amewataka Mikel Arteta na mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Edu kumsajili Ivan Toney katika dirisha hili ikiwa wanahitaji kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu.

Arsenal baada ya kukosa taji la Ligi Kuu England msimu uliopita moja kati ya maeneo ambayo yaliripotiwa kuwaangusha ilikuwa ni ushambuliaji.

Petit anaamini Arsenal inahitaji mshambuliaji atakayeweza kufunga mabao 20 au zaidi ili kuinyang’anya taji Man City na staa huyo kwa sasa anaamini ni Toney ambaye anawindwa na Chelsea pia.

Tangu kuanza kwa Ligi Kuu England msimu huu, Arsenal imeshinda mechi zote mbili za kwanza za ligi ikiibamiza Wolves na Aston Villa lakini Petit bado haoni kama inaweza kuchukua ubingwa ikiwa itaendelea na kikosi ilichonacho kwa sasa.

Katika dirisha hili la usajili, washika mitutu hao wamewasajili mastaa kadhaa kama kiungo Mikel Merino na beki wa kati Riccardo Calafiori pia ikimsainisha mkataba wa kudumu kipa David Raya baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesha wakati anaichezea kwa mkopo msimu uliopita.

Licha ya ushauri ambao Petit ameutoa taarifa za ndani kutoka tovuti ya Daily Mail zinadai mpango wa Arsenal kumsajili Toney utakuwa mgumu sana kwa sababu staa huyo amepokea ofa nono kutoka Saudi Arabia.

Toney ambaye anawindwa na timu mbalimbali duniani amepokea ofa ya mshahara wa Pauni 400,000 kwa wiki kutoka Al Ahli.

“Arsenal inahitaji mshambuliaji atakayewafungia mabao 20 kwa msimu, kwa sasa ina wachezaji wachache ambao wanaweza kufunga mabao 10 hadi 15.”

Chanzo: Mwanaspoti