Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yapeleka mtu kutazama majembe mapya

Bosi Wa Zamani Wa Arsenal Adai Arteta 'amechafua Picha Ya Klabu' Arsenal yapeleka mtu kutazama majembe mapya

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal imeripotiwa kutuma skauti wake kwenda kuwatazama mastaa wawili wa Sporting Lisbon, straika Viktor Gyokeres na beki wa kati Ousmane Diomande.

Arsenal ilionyesha dhamira ya dhati ya kunasa huduma ya straika mpya kwenye dirisha la Januari, lakini kipindi hicho kilipita bila ya miamba hiyo ya Emirates kuongeza mchezaji yeyote kutokana na kubanwa na Financial Fair Play.

Hata hivyo, Arsenal inatazamiwa kufanya usajili wa straika mpya kwa sababu ndio eneo linalopewa nafasi kubwa kwenye mipango yao ya usajili wakati wa dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Chaguo la kwanza la Arsenal kwenye nafasi ya straika kwa sasa ni Gabriel Jesus, ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, wakati mshambuliaji mwenzake Eddie Nketiah ameshindwa kumshawishi kocha Mikel Arteta na kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha miamba hiyo.

Wakati Arsenal ikisaka straika mpya, Gyokeres anatajwa kwenye orodha ya wakali wanne wanaowindwa na miamba hiyo ya Emirates. Hivyo, Arsenal ilituma skauti wake kumtazama Gyokeres na mwenzake Diomande katika mchezo mkali dhidi ya Benfica. Katika mechi hiyo, Gyokeres alifunga bao la pili kwenye ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Sporting katika mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Ureno.

Fowadi huyo wa kimataifa wa Sweden aliendeleza moto wake baada ya kufunga tena juzi Jumapili kwenye ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Farense kwenye Primeira Liga.

Kutokana na hilo, Gyokeres sasa amefunga mabao 32 katika mechi 35 za kiushindani alizochezea timu hiyo tangu alipojiunga kutoka Coventry City wakati wa dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

Kwenye mkataba wake, Gyokeres imeelezwa inahitaji kulipwa Pauni 86 milioni ili kuvunja mkataba huo, ambao utafika kikomo kwenye kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2028.

Chanzo: Mwanaspoti