Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yamtega leroy Sane

Leroy Sane 2324 65cf58f864ef7 Leroy Sane

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mambo ni moto. Arsenal imeanza kumfuatilia kwa karibu winga Leroy Sane na kutazama uwezekano wa kunasa saini yake dirisha hili.

Arsenal inahitaji huduma ya winga huyo ili kuboresha safu yao ya ushambuliaji, huku ikitaka pia kuleta mtu wa kuja kumpa ushindani Bukayo Saka.

Katika msako wao wa winga mpya, miamba hiyo inayonolewa na Mikel Arteta, inaamini mkali huyo wa Bayern Munich, Sane, mwenye uzoefu pia wa kukipiga Ligi Kuu England, atajiunga kwenye timu yao.

Mkataba wa Sane huko Bayern, unaripotiwa kukaribia ukingoni huku mazungumzo ya dili jipya yakidaiwa kukwama. Hilo ndilo linalowafanya Arsenal kufuatilia dili hilo kwa karibu zaidi ili kumsajili staa huyo wa zamani wa Manchester City.

Sane, 28, mkataba wake huko Allianz Arena umebakiza mwaka mmoja tu, huku Arteta akifahamiana vyema na Sane kwa kuwa pamoja Etihad.

Sane alijiunga na Bayern kwa ada ya Pauni 55 milioni kutokea Man City mwaka 2020. Anachotaka Mjerumani huyo kubaki Ujerumani, lakini hilo pia aliondoi uwezekano wa kuhama kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Aprili mwaka huu, Sane alisifu mavitu ya Arteta aliposema: “Nilikuwa na furaha sana kwa kufanya naye kazi. Alinisaidia mengi sana. Tulikuwa na vikao vya ana kwa ana juu ya kuboresha kiwango cha soka langu.”

Jumatatu iliyopita, Arsenal ilitangaza kukamilisha usajili wa beki wa Bologna, Riccardo Calafiori, aliyemnasa kwa ada ya Pauni 42 milioni. Usajili wa beki huyo Mtaliano ni unafanya kuwa mchezaji wa pili kunasa kwenye dirisha hili baada ya kipa David Raya akitokea Brentford kwa Pauni 27 milioni. Ukimweka kando Sane, Arsenal imeripotiwa kumsaka pia winga wa Hispania na bingwa wa Euro 2024, Nico Williams.

Chanzo: Mwanaspoti