Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yamgeukia Havertz

Kai Havert Tz Kai Havertz

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Arsenal inafanya mazungumzo na mchezaji wa Chelsea raia wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz kwajili ya kumsajili katika dirisha hili kubwa.

Arsenal wanataka kuwasilisha ofa kwa klabu ya Chelsea kwajili ya kumnunua kiungo huyo wa kijerumani Kai Havertz ambaye amekua hana msimu mzuri hivi karibuni na mchezaji mwenyewe anataka kuondoka ndani ya timu hiyo.

Washika mitutu wa London wanataka kuwasilisha dau mezani kwa ajili ya Havertz pamoja na kiungo wa klabu ya West ham United ambaye wamekua wakimfukuzia kwa muda mrefu Declan Rice ili kuboresha timu yao kuelekea msimu ujao.

Kai Havertz alikua akihitajika na klabu ya Real Madrid lakini mpaka sasa inaonekana wababe hao wa soka nchini Hispania wamejitoa katika mbio hizo, Huku Arsenal sasa wakiuonesha nia ya dhati ya kumchukua kiungo huyo.

Arsenal wanataka kuboresha timu yao zaidi baada ya kua na msimu mzuri mwaka 2022/23 licha ya kukosa ubingwa wakiamini kama wataboresha timu yao basi wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi msimu ujao na hata kubeba ubingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live