Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yamfungia kazi Victor Boniface

Boniface1 Victor Boniface

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

HABARI ndo hiyo. Arsenal imeripotiwa kukoleza moto kwenye mpango wao wa kunasa huduma ya straika wa Bayer Leverkusen, Victor Boniface kabla ya dirisha hili la Januari halijafungwa.

Baada ya msimu mmoja wa kuwa kwenye kikosi cha Union SG ya Ubelgiji, Boniface alinaswa na Leverkusen kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa ada ya Euro 20 milioni na tangu hapo amekuwa moto kwelikweli kwa kutikisa nyavu huko Ujerumani.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 22 amefunga mabao 16 na kuasisti mara mbili katika mechi 23 alizochezea Leverkusen katika michuano yote msimu huu, ikiwamo mabao 10 katika mechi 16 za Bundesliga.

Boniface amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Xabi Alonso, kikiongoza msimamo wa Bundesliga kwa tofauti ya pointi saba na hakijapoteza mechi yoyote kati ya 27 za mwisho ilizocheza kwenye michuano yote msimu huu.

Staa huyo wa kimataifa wa Nigeria kwa sasa yupo nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli ya korodani iliyomfanya ashindwe kucheza fainali za Afcon 2023 zinazoendelea huko Ivory Coast, lakini hilo haliwazuii Arsenal kwenye mpango wao wa kutaka kumsajili.

Real Madrid inafahamika wazi inamtolea macho straika Boniface, huku Chelsea na West Ham United zikiamini ni mchezaji ambaye anastahili kwenda kucheza kwenye vikosi vyao.

Hata hivyo, Arsenal wanaonekana kuwa siriazi kwenye mchakamchaka wa kuhitaji straika kwenye dirisha hili baada ya Gabriel Jesus na Eddie Nketiah kushindwa kufanya mambo ya maana kwenye timu hiyo.

MASTRAIKA WENGINE KWENYE RADA ZA ARSENAL HAWA HAPA

-Ivan Toney (Brentford)

-Victor Osimhen (Napoli)

-Joshua Zirkzee (Bologna)

-Youssef En-Nesyri (Sevilla)

-Benjamin Sesko (RB Leipzig)

-Serhou Guirassy (VtB Stuttgart)

-Roberto Firmino (Al-Ahli)

-Gabriel Barbosa (Flamengo)

Chanzo: Mwanaspoti