Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yakubali unyonge mbele ya Man City

Riyad Mahrez Pe Mahreza akiifungia City kwa kwaju wa Penati

Sat, 1 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester City imelazimika kutokea nyuma kwa bao 1-0 na kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Arsenal katika mechi ya Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Emirates.

Arsenal walitangulia kupata goli kupitia kwa Bukayo Saka akimalizia pasi ya Martinell katika mchezo ambao The Gunners walilazimika kumaliza mchezo kabla ya dakika 90 kufuatia Gabriel Magalhaes kuonyeshwa kadi nyekundu.

Ushindi huo unaifanya Manchester City kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya alama 11 ambapo kesho Jumapili kutakuwa na mchezo baina ya Chelsea na Liverpool.

Rekodi zinaonyesha kuwa hakuna timu ambayo ilishindwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England ikiwa imeanza na ushindi katika mechi ya kwanza ya Ligi ukiwa ni mwaka mpya.

Mabao ya Man City yakiwekwa kimiani na Riyard Mahrez kwa penati huku bao la ushindi likifungwa dakika za nyongeza kabisa kupitia kwa Rodri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live