Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yakataa straika

IMG 4098 Ivan Toney.jpeg Mshambuliaji wa klabu ya Brentford Ivan Toney

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal haina mpango wa kutoa Pauni 100 milioni katika dirisha hili ili kumsajili straika wa Brentford na England Ivan Toney, 27. Kiasi hicho cha Pauni 100 milioni ndicho kinachohitajika na mabosi wa Brentford ili kumuuza.

Mabosi wa Arsenal wanaamini kiasi hicho cha pesa ni kikubwa zaidi hivyo wamepanga kusubiri hadi mwisho wa msimu huu ambapo atakuwa amebakisha msimu mmoja, hivyo wataweza kumpata kwa kiasi kidogo cha pesa.

Arsenal imekuwa kwenye uhitaji wa straika kwa sababu inataka kuboresha eneo lao la ushambuliaji linaloonekana kuwa na mapungufu.

Brentford inadaiwa kuwa tayari kumuuza fundi huyu lakini sio dirisha hili, kwani bado ina mpango wa kutaka kumtumia.= Mkataba wa sasa wa fundi huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2025. Msimu uliopita alicheza mechi 35 za michuano yote na kufunga mabao 21.

Chanzo: Mwanaspoti