Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yakabidhiwa ubingwa England

Ubingwa EPL.png Arsenal yakabidhiwa ubingwa England

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Mkongwe wa soka na mchambuzi wa kituo cha televisheni cha Sky Sports, Roy Keane amesema Arsenal ina uwezo wa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu endapo Man City itashindwa kuendeleza ubabe.

Kikosi cha kocha Pep Guardiola kwa sasa kinashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi tatu kutoka kwa vinara Arsenal na pointi moja nyuma ya Liverpool baada ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Tottenham.

Keane anaihofia Man City akidai haionyeshi kuwa ina njaa kama ilivyokuwa msimu uliopita ilipobeba mataji matatu, hata hivyo amesisitiza itakuwa ujinga kuitabiria timu ambayo ishavuna mafanikio makubwa.

Baada ya mechi ya Spurs na Man City kumalizika, Keane alisema: “Nisingeweka dau dhidi ya Man City, lakini nimeanza kuwa na shaka kutokana na kiwango chao msimu huu.”

Aliendelea kwa kusema: “Kuna sababu, ndo maana Man City haikubeba ubingwa miaka minne mfululizo, hii inasababisha wachezaji kuwa na njaa ya mafanikio, hakuna majeraha kwenye timu, na ubora wa wachezaji kwa ujumla, lakini ukiangalia Arsenal na Liverpool zimeonyesha zina nguvu sana, Arsenal imekuja kwa kishindo baada ya kukaribia ubingwa msimu uliopita.”

Naye mkongwe wa Liverpool, Jamie Carragher alikubaliana na kauli ya Keane, akisisitiza Arsenal itakuwa na ushindani katika mbio za kuwania msimu huu, ikifuatiwa na Liverpool iliyobeba ndoo hiyo mwaka 2019.

Carragher alisema: “Ukituuliza nadhani kila mtu anatamani kuona Man City ikibeba ubingwa, Tumeona msimu uliopita, Man City ilikuwa inashinda mechi zake mfululizo tofauti na timu nyingine, nadhani Arsenal ina nguvu sana msimu huu.”

Carragher aliendelea kusema kuwa ana furaha kuona wachezaji wa Arsenal na Liverpool wakiipa changamoto Man City kwani inafanya mbio za ubingwa kuwa za kusisimua zaidi kwa mashabiki msimu huu.

Carragher akamchimba mkwara mchambuzi mwenzake Micah Richards ambaye aliwahi kukipiga Man City: “Najua Micah Richards hutaki kusikia kauli hizi, hatuegemei upande wowote, ni vizuri kuona Man City ikipoteza pointi. Kwa vile msimu uliopita ulibeba makombe matatu.”

Chanzo: Dar24