Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yakaa pazuri kwa Sesko

Benjamin Sesko Benjamin Sesko

Sat, 18 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal ipo namba moja kwenye msururu wa timu zinazofukuzia saini ya straika wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, ikitaka huduma kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Fowadi huyo wa kimataifa wa Slovenia amekuwa na kiwango bora sana huko Bundesliga.

Sesko alihamia RB Leipzig mwaka jana na amefunga mabao 13 kwenye mechi 30 Bundesliga. Na kinachoelezwa, Arsenal ipo kwenye wakati mzuri wa kumnasa fowadi huyo mwenye kimo cha futi 6 na inchi 5.

Huko nyuma ilielezwa fowadi huyo wa zamani wa RB Salzburg kwenye mkataba wake kimewekwa kipengele kinachohitaji ililipwa Pauni 43 milioni kwa timu itakayohitaji kunasa saini yake. Na kiwango hicho kinaelezwa kwamba kimeongezeka na kufikia Pauni 64 milioni.

Sesko amefunga kwenye kila mechi katika michezo sita iliyopita, ikiwamo bao dhidi ya Borussia Dortmund, iliyotinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu. Wakala wake, Elvis Basanovic alikuwapo uwanjani wakati Arsenal inaichapa Chelsea 5-0 mwezi uliopita.

Manchester United nayo imekuwa ikiripotiwa kuhitaji saini ya Sesko, wakitafuta mchezaji wa kumsaidia Rasmus Hojlund. Arsenal ilifanikiwa duru la pili la msimu huu, wakati kocha Mikel Arteta alipomtumia Kai Havertz kama straika.

Hilo linawafanya Arsenal kuwa na ulazima wa kuingia sokoni kwenye dirisha lijalo kusajili straika halisi. Ukimweka kando Sesko, washambuliaji wengine wanahusishwa na The Gunners ni Viktor Gyokeres na Joshua Zirkzee.

Chanzo: Mwanaspoti