Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yajitosa tena kwa Dusan Vlahovic

Vlhovic.png Arsenal yajitosa tena kwa Dusan Vlahovic

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: Dar24

Klabu ya Juventus ya Italia inatarajiwa kumweka sokoni Mshambuliaji wao Dusan Vlahovic dirisha lijalo na Arsenal ni moja ya timu zinazoweza kutuma ofa kwa ajili ya kumsajili nyota huyo.

Vlahovic alikuwa akihusishwa kuondoka tangu dirisha lililopita na Juventus ilikuwa ikihitaji kiasi kisichozidi Pauni 34 milioni ili kumuuza na iliripotiwa pia walitaka kufanya mabadilishano ya nyota huyu na Romelu Lukaku aende Juve na Vlahovic akacheze Chelsea.

Hata hivyo, sasa Juve inataka kumuuza mapema nyota huyo kwani msimu ujao mshahara wake utapanda na kufikia Pauni 10 milioni jambo wanaloona litawatia hasara kwa sababu staa huyu pia muda mwingi amekuwa hachezi kutokana na majeraha ya mara kwa mara.

Arsenal ilikuwa tayari kutoa Pauni 88 milioni dirisha la usajili la Januari mwaka jana lakini wakafeli na Juventus ikashinda vita, ingawa bado inapambana kupata huduma yake.

Katika mechi 66 alizocheza Juventus, Vlahovic amefunga mabao 25, rekodi ambayo haikutazamiwa wakati anajiunga na Juve.

Chanzo: Dar24