Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yajipeleka kundi la kifo UEFA 2023/24

Arsenal Europa Kikosi cha Arsenal

Fri, 19 May 2023 Chanzo: Dar24

Arsenal itarejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2016-17.

Arsenal imejiweka pagumu kwenye nafasi ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, lakini mashabiki wake sasa wamepata matumaini mapya ya kuwaona wakicheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Lakini, shida kwa kocha Mikel Arteta na chama lake, anapaswa kujiandaa mapemą kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wakapangwa kwenye Kundi la Kifo katika mikiki mikiki hiyo ya kusaka ubingwa wa Ulaya.

Kutokana na kushindwa kushíriki michuano ya Ulaya kwa miaka ya karibuni, Arsenal ina uwezekano mkubwa wakawekwa kwenye Pot 3 wakati wa upangaji wa makundi mwezi Agosti.

Na kama ikiwa hivyo, basi Arsenal itakuwa na shughuli pevu kweli kweli katika mpango wao wa kupenya hatua hiyo ya makundi na kuingia mtoano.

Chungu cha Kwanza (Pot 1) kitakuwa na timu zenye viwango vikubwa, ikiwamo mabingwa wakutoka Ligi Kuu tano bora za Ulaya na bingwa wa Europa League.

Jambo hilo linaweza kuwafanya Arsenal kupangwa kundi moja na Bayern Munich, ambao waliwafanyia udhalilishaji mkubwa mara yao ya mwisho walipokuwapo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Bayern Munich waliichapa Arsenal jumla ya mabao 10-2 mwaka 2017 kipindi hicho wakiwa chini ya kocha Arsene Wenger.

Timu nyingine zitakazokuwa kwenye Pot l ambazo huenda mojawapo ikapangwa na Arsenal ni PSG, Barcelona na Napoli. Hawatapangwa na Manchester City kwa kuwa wanacheza kwenye ligi moja.

Chungu cha Pili (Pot 2) kinaweza kuwa na Real Madrid ambazo zinaweza kupangwa na Arsenal, huku kwenye Chungu cha Tatu (Pot 3) itakuwa na Shakhtar Donetsk, RB Salzburg na SS Lazio kwa kuzitaja kwa uchache.

Chanzo: Dar24