Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yajipanga kivingine kwa Bruno Guimaraes

Bruno Guimaraes.jpeg Bruno GuimarĂ£es Rodriguez

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal inafikiria kuwasilisha ofa ya pesa na mchezaji kwenda Newcastle ili kuipata saini ya kiungo wa timu hiyo na Brazil, Bruno Guimaraes, 26, dirisha hili.

Mabosi wa Arsenal wanahitaji kusajili kiungo dirisha hili na kwa mujibu wa taarifa kocha wao Mikel Arteta ndiye aliyependekeza jina la Bruno lakini changamoto ni bei yake inayodaiwa kufikia Pauni 100 milioni.

Ili kupunguza makali ya bei yake hiyo, Arsenal imepanga kumjumuisha mmoja wa wachezaji wao na pesa kidogo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Footballtransfer, Newcastle ipo tayari kukubali dili hilo kwa sababu imeshapanga kumuuza Bruno.

Haijajulikana ni mchezaji gani atakuwa sehemu ya ofa hiyo ingawa kuna mastaa ambao Arsenal ipo karibu kuachana nao katika dirisha hili ikiwa pamoja na Oleksandr Zinchenko, Emile Smith Rowe, Albert Sambi Lokonga, Eddie Nketiah na Thomas Partey.

Arteta amedhamiria kulipeleka kombe la Ligi Kuu England Emirates baada ya kuhangaika kulisaka kwa muda mrefu.

Chanzo: Mwanaspoti