Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yajaribu bahati kwa Osimhen

Victor Osimhen.jpeg Arsenal yajaribu bahati kwa Osimhen

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal mpango wao wa kunyakua taji la Ligi Kuu England upo palepale na ndio maana ipo kwenye mikakati kabambe kabisa ya usajili.

Wakati dirisha la usajili la kipindi hiki cha majira ya kiangazi huko Ulaya likipamba moto, kinachoelezwa ni kwamba Arsenal imeingia kwenye mchakato wa kuwania saini ya mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen.

Ripoti kutoka Italia kupitia Team Talk, Arsenal imeweka wazi mpango wa kunasa saini ya Mnigeria huyo, ambaye yupo tayari kwenda kukipiga kwenye Ligi Kuu England.

Arsenal inahitaji straika wa kiwango cha dunia ili kukamilisha mpango wao wa kubeba taji la Ligi Kuu England, ambalo ilishindwa kulinyakua kwa misimu miwili iliyopita katika dakika za mwisho kabisa.

Miamba hiyo ya Emirates inayonolewa na Mikel Arteta inaamini ikipata straika wa maana itafanikiwa kwenye mpango wao wa kunyakua taji la Ligi Kuu England. Kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ilijaribu kumsajili straika wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, lakini ilikwama baada ya staa huyo kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki kwenye kikosi hicho cha wababe wa Bundesliga.

Na sasa, Arsenal inaripotiwa kuhamia kwa Osimhen, wakiamini ni mshambuliaji anayefaa kuja kuwapa nguvu katika kushindana na Manchester City ankwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England, ambapo hawajabeba taji hilo kwa zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Awali baada ya Sesko kuwaangusha, Arsenal ilielekeza nguvu kwa straika wa Girona, Artem Dovbyk, kinara wa mabao kwenye LaLiga kwa msimu uliopita baada ya kufunga mabao 24.

Lakini, sasa kinachoelezwa wanamtazama straika wa daraja la juu, Osimhen kuwa ndiye sahihi wa kwenda kumaliza shida zao na hivyo kuwa na uwezo wa kuzipiga vikumbo timu kubwa kama Man City kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

Chanzo: Mwanaspoti