Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yaiwahi Juve kwa Riccardo Calafiori

Riccardo Calafiori Riccardo Calafiori

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi za usajili za kimataifa zinasema Arsenal iko mbele ya Juventus katika kumfuatilia beki wa Bologna Riccardo Calafiori, 22, ambaye ameng'ara katika kikosi cha Italia kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2024). (Telegraph) Newcastle United ina nia kumsajili fowadi wa Nottingham raia wa Sweden Anthony Elanga,22. (Teamtalk)

Real Madrid inaitaka saini ya beki wa Crystal Palace, Marc Guehi, 23 huku Barcelona na Juventus pia zikimfuatilia. (Sun)

Beki wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 24, anapendelea kuhamia Manchester United. Bayern Munich imemweka De Ligt katika thamani ya pauni mil 42.4. (Sky Sports) Paris Saint-Germain imeulizia kuhusu upatikanaji wa fowadi wa Leeds United, Crysencio Summerville,22. (De Telegraaf - in Dutch)

Brighton & Hove Albion ina nia kuwasajili kiungo wa Feyenoord raia wa Uhoalnzi Mats Wieffer,24 na beki wa wa Rayo Vallecano raia wa Romania Andrei Ratiu, 26. (Athletic).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live