Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yaikataa European Super League

Arsenali.png Arsenal yaikataa European Super League

Sun, 24 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta amesema ni muhimu kuwakumbatia mashabiki huku klabu yake ikikataa kushiriki katika pendekezo lililorekebishwa la European Super League (ESL).

Arsenal walikuwa miongoni mwa klabu 12 vilivyoungana na mpango wa awali wa ESL mwaka 2021.

Alhamisi (Desemba 21) Mahakama ya Ulaya ya Haki ilipiga marufuku klabu kujiunga na ESL kwa kuwa kinyume cha sheria lakini ligi iliyorekebishwa ilipendekezwa saa chache baadae.

“Wafuasi wa mpira wa miguu na shauku wanayoleta kwenye michezo ndio sababu mchezo huu ni wao,” alisema Arteta.

“Maoni yao ni muhimu sana na lazima tuwatunze,” aliongeza.

Mwaka wa 2021, timu 12 zilijitenga na kukataa kujisajili na ESL iliyoundwa kushindana na mashindano ya Uefa, lakini mradi huo ulikosolewa na mashabiki, vikundi vya mashabiki, ligi za ndani za Ulaya na hata serikali na kusababisha kuanguka kwa pendekezo hilo ndani ya saa 72.

Miongoni mwa klabu 12 ni Real Madrid na Barcelona pekee ndio waliokubaliana na ligi iliyopendekezwa na A22- huku vingine vikirudi nyuma.

The Gunners wamejunga na Chelsea, Tottenham, Manchester City na Manchester United katika kutangaza kwamba msimamo wao haujabadilika juu ya ESL na kuthibitisha kujitolea kwao kwa mashindano ya UEFA.

“Tunabaki katika nafasi ileile na tunapenda kucheza Ligi ya Mabingwa na tutaendelea kufanya hivyo,” alisema Arteta.

“Mazungumzo (na wamiliki) tuliyokuwa nayo yalikuwa wazi baada ya yale yaliyotokea miaka miwili iliyopita. Nadhani klabu imetoa tamko ambalo ni wazi na lina uwazi. Tutasimamia hilo.”

Pendekezo jipya ni mfumo wa ligi ambao ungejumuisha timu 64 za wanaume na timu 32 za wanawake na uwezo wa kila mwaka wa kupanda na kushushwa daraja.

Chanzo: Dar24