Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yahofiwa kurudia kosa

Image 591 1140x640.png Arsenal yahofiwa kurudia kosa

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: Dar 24

Beki na nahodha msaidizi wa zamani wa Arsenal Kolo Toure anaamini mastaa wa klabu hiyo ya jijini London kama Bukayo Saka na Gabriel Martinelli wataendelea kubaki Emirates baada ya sasa kuibuka kwa hofu ya kwamba huenda wakapigwa bei kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Arsenal inafurahia msimu bora chini ya kocha Mikel Arteta, ikiongoza ligi kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya Manchester City, lakini The Gunners wamecheza michezo miwili zaidi.

Mafanikio yao yamechangiwa na vijana wachanga kabisa waliopo kwenye kikosi chao.

Mashabiki wa Arsenal wamekuwa na hofu kwamba wachezaji wao bora wanaweza kuuzwa kama ambavyo klabu hiyo imekuwa ikifanya inaposhindwa kuwaridhisha wachezaji hao kwa kubeba mataji.

Toure, Gael Clichy, Emmanuel Adebayor na Samir Nasri wote waliondoka Emirates kwenda Etihad kati ya mwaka 2009 na 2011 mwanzoni mwa zama za utawala wa Sheikh Mansour huko Man City.

Tangu wakati huo, Man City imeshinda mataji sita ya Ligi Kuu England, huku wakifukuzia la saba msimu huu na Arsenal walitoka patupu kwenye misimu 19, ambapo mara ya mwisho msimu wa 2003/04, wakati huo Toure alikuwa akiichezea Arsenal.

Saka, kwa mfano mkataba wake utafika tamati Juni na Toure anaamini staa huyo pamoja na Martinelli watabakizwa klabuni hapo.

Toure amesema: “Hii nina hakika haitatokea, Edu na Arteta wanajua kitu cha kufanya. Wamekuwa kwenye soka kwa muda mrefu, hivyo wanafahamu umuhimu wa kuwafanya wachezaji kuwa pamoja kwa muda mrefu. Wanahitaji kuilinda timu yao kwa miaka mitatu au zaidi ili kuwa na ubora mkubwa ndani ya uwanja.”

Chini ya uongozi wa mkurugenzi wa michezo Edu, Arsenal imeunda kikosi matata kabisa cha vijana wengi. Saka (21), Martinelli (21), Eddie Nketiah (23), Jakub Kiwior (23), Takehiro Tomiyasu (24), Fabio Vieira (22), Reiss Nelson (23), Emile Smith Rowe (22), Aaron Ramsdale (24) na nahodha Martin Odegaard (24) ambapo wote wapo kwenye umri wa ujana wa kupambana 2003/04, uwanjani.

Chanzo: Dar 24