Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yaendeleza ushindi Europa

WhatsApp Image 2022 10 07 At 9.jpeg Arsenal yaendeleza ushindi Europa

Fri, 7 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Washika mitutu wa London, Klabu ya Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bodo/Glimt ya Norway katika mchezo wa Kundi A UEFA Europa League jana usiku Uwanja wa Emirates Jijini London.

Mabao ya Arsenal yamefungwa na Eddie Nketiah dakika ya 23, Rob Holding dakika ya 27 na Fabio Vieira dakika ya 84 na kwa ushindi huo katika mchezo wake wa pili, The Gunners inafikisha pointi sita na kupanda kileleni mwa Kundi, ikiizidi pointi mbili Bodø/Glimt iliyocheza mechi moja zaidi.

Baada ya ushindi wa 5-1 dhidi ya wenyeji, FC Zurich sasa PSV nayo ina pointi nne katika nafasi ya tatu, ikizidiwa wastani wa mabao na Bodo/Glimt.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live