Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yaanza kuota Ubingwa wa EPL

Gunners Arsenal.jpeg Arsenal yaanza kuota Ubingwa wa EPL

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mikel Arteta anahisi Arsenal "imepiga hatua nyingine" baada ya ushindi muhimu wa 'dabi' dhidi ya Tottenham Hotspur uliowafanya kuwa pointi nane zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester City inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 39.

Hugo Lloris alijifunga kabla ya Martin Odegaard kuongeza la pili huku utawala wa Arsenal katika kipindi cha kwanza ukiwapa ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur, Jumapili.

Hilo liliwaacha Arsenal wakiwa na uongozi wa pointi nane kileleni mwa Ligi Kuu ya England na Arteta anaamini kuwa timu yake ilidhihirisha kuwa inawania taji.

Arteta aliiambia Sky Sports: "Nilipenda jinsi tulivyocheza na ujasiri tulioonyesha kuja hapa na kucheza.

"Tukifanya kazi yetu tunaweza kuwafurahisha watu wengi na nina uhakika tumewafurahisha sana mashabiki wa Arsenal. Kila kitu tunachouliza, wako tayari kujaribu kufanya.

"Ni kundi la wachezaji wa kutisha, nadhani leo (juzi), tumepiga hatua nyingine, tulishinda msimu uliopita kwenye viwanja vikubwa, lakini jinsi tulivyoshinda ilikuwa ya kupendeza kutazama.

"Inaonyesha si tu dhamira na ujasiri, lakini lazima uwe na imani na ubora wa kufanya hivyo dhidi ya timu hii. Hilo linategemea kabisa wachezaji.

"Tulikuwa wakali sana. Tulikuwa wakali sana dhidi ya wachezaji wa hali ya juu. Tulishinda mipira mingi na pambano. Walitengeneza nafasi kadhaa, ni timu hatari, lakini tulifanya kazi nzuri."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live