Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal wauweka Ubingwa rehani, wachapwa bao 2 Emirates

Saka X Rice Vs Villa Arsenal wauweka Ubingwa rehani, wachapwa bao 2 Emirates

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matumaini ya Arsenal kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England yameanza kupangua baada ya jana Jumapili kuchapwa mabao 2-0 nyumbani na Aston Villa Uwanja wa Emirates Jijini London.

Mabao yaliyozamisha Arsenal yamefungwa na kiungo Mjamaica, Leon Bailey dakika ya 84 na mshambuliaji Muingereza, Ollie Watkins dakika ya 87.

Kwa ushindi huo, Aston Villa inafikisha pointi 60 katika mchezo wa 33 na kupanda nafasi ya nne, ikiizidi tu wastani wa mabao Tottenham Hotspur ambayo imecheza mechi 32.

Kwa upande wao Arsenal baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao 71 nafasi ya pili wakiizidi wastani wa mabao Liverpool na wote wakiwa nyuma ya Manchester City wenye pointi 73 baada ya timu zote kucheza mechi 32.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live