Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal warudi kwenye anga za Ubingwa EPL

IMG 6264.jpeg Arsenal waliichapa Burnley 3-1

Sun, 12 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumamosi Uwanja wa Emirates Jijini London.

Mabao ya Arsenal yamefungwa na Leandro Trossard dakika ya 45 na ushei, William Saliba dakika ya 57 na Oleksandr Zinchenko dakika ya 74, wakati la kufuatia machozi la Burnley limefungwa na Josh Brownhill dakika ya 54.

Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Manchester City ambao wamecheza mechi 11, wakati Burnley inabaki na pointi zake nne za mechi 12 nafasi ya 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live