Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal warudi kileleni EPL

Odegaard EPL Arsenal warudi kileleni EPL

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Arsenal jana imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Wolverhampton Wanderers Uwanja wa Molineux mjini Wolverhampton, West Midlands.

Mabao ya mshambuliaji Mbelgiji, Leandro Trossard dakika ya 45 na kiungo Mnorway, Martin Ødegaard dakika ya 90'+5 na kwa ushindi huo, Arsenal wanafikisha pointi 74 katika mchezo wa 33 na kurejea kileleni wakiwazidi pointi moja tu mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wana mechi moja mkononi.

Kwa upande wao Wolverhampton Wanderers baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao43 za mechi 33 nafasi ya 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live