Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal wao ni Gyokeres tu

Sporting Lisbon Viktor Gyokeres Photo 1 Arsenal wao ni Gyokeres tu

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Hakuna namna. Arsenal mpango wao kwa sasa ni kunasa huduma ya straika wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres, wanayeamini atawagharimu Pauni 60 milioni.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anahitaji huduma ya straika mpya dirisha hili.

Hata hivyo, klabu hiyo ya Ureno imedaiwa kuweka ngumu kimtindo, ikisisitiza huduma ya mkali huyo wa kimataifa wa Sweden haipatikani bila Pauni 85 milioni kama kinavyoeleza moja ya vipengele vilivyopo kwenye mkataba wake.

Gyokeres, 26, alikuwa na kiwango bora sana msimu wa 2023-24, alifunga mabao 43 na kuasisti mara 15 katika mechi 50 alizocheza kwenye michuano yote. Kiwango chake bora kimeifanya Sporting kunyakua ubingwa Primeira Liga, huku pia akiibuka kinara wa mabao kwenye ligi hiyo akiwa amefunga mara 29.

Kocha Arteta anahitaji kuboresha safu yake ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu ujao na anamtazama Gyokeres kama mchezaji mwafaka atakayekwenda kufiti kwenye kikosi chake. Awali alihitaji saini ya straika wa RB Leipzig, Benjamin Sesko na ilikuwa tayari kulipa Pauni 55 milioni kunasa saini ya mchezaji huyo, lakini staa huyo aliamua kubaki zake kwenye klabu hiyo ya Bundesliga na kusaini mkataba mpya.

Arsenal imekuwa ikimfuatilia Gyokeres kwa zaidi ya mwaka na kujihakikishia atakuja kuongeza kitu kwenye fowadi yao.

Licha ya kwamba bei yake iliyoandikwa kwenye mkataba ni Pauni 85 milioni, Arsenal inaamini inaweza kumpata kwa gharama ya chini na kumnyakua fowadi huyo wa zamani wa Coventry City.

Gyokeres alisema kuhusu hatima yake: “Kubaki msimu ujao? Hii ni soka, ni kawaida siwezi kuahidi kitu. Ningependa sana kubaki hapa, lakini kwenye soka kitu chochote kinaweza kutokea, tena kinatokea kwa haraka. Siwezi kutabiri, ngoja tuone.”

Sporting Lisbon inataka pesa kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi na inaweza kupata kwa kuuza mastaa wake, wakiwamo mabeki Ousmane Diomande na Goncalo Inacio, ambao wamekuwa wakihusishwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu England, ikiwamo Arsenal.

Chanzo: Mwanaspoti