Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal wampiga mtu bao 5 EPL

IMG 6132.jpeg Eddie Nketiah alipiga hat-trick

Sun, 29 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Washika mitutu wa London, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumamosi Oktoba 28 Uwanja wa Emirates Jijini London.

Nyota wa mchezo wa huo alikuwa ni mshambuliaji Muingereza Edward ‘Eddie’ Keddar Nketiah mwenye asili ya Ghana ambaye amefunga mabao matatu dakika za 28, 50 na 58, wakati mabao mengine ya Arsenal yamefungwa na Fabio Vieira dakika ya 88 kwa penalti na Takehiro Tomiyasu dakika ya 90 na ushei.

Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 24 na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili tu na vinara, Tottenham Hotspur, wakati Sheffield United inabaki na pointi yake moja mkiani baada ya wote kucheza mechi 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live