Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal waipiga chini ofa ya Folarin Balogun

Folarin Balogun 1140x640 Folarin Balogun

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Klabu ya Arsenal imekataa ofa ya Klabu ya AS Monaco kwa ajili ya mshambuliaji Folarin Balogun, lakini imekubaliana kuhusu Mkataba ambao utamfanya mchezaji mwenzake wa Kimataifa wa Marekani, Matt Turner, ajiunge na Nottingham Forest, vyanzo vimeiambia ESPN.

Klabu hiyo ya Ligi Kuu England inamthaminisha Balogun kwa takriban Euro Milioni 58 na inafilkiriwa kuwa tayari kumruhusu kuondoka kwa bei inayofaa, huku Inter Milan pia ikitarajiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kuwania saini yake.

Balogun amebakiza miaka miwili katika mkataba wake na Arsenal na angependelea kuhama kwa uhamisho wa kudumu ikizingatiwa uwezekano wa kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza kwenye Uwanja wa Emirates, hata baada ya jeraha la goti litakalomfanya Gabriel Jesus kuwa nje ya uwanja kwa majuma kadhaa ya kwanza ya msimu.

Balogun mwenye umri wa miaka 22, hakuwa sehemu ya kikosi cha siku ya mechi kilichoshinda Ngao ya Jamii Jumapili (Agosti 06) dhidi ya Manchester. City kwenye Uwanja wa Wembley baada ya kuwa nje ya uwanja kutokanana tatizo la mguu.

Balogun alicheza kwa mkopo katika Klabu ya Ligue 1 ya Reims msimu uliopita, akifunga mabao 21 katika mechi 34 alizocheza, lakini yuko nyuma ya mchezaji mpya Kai Havertz na Eddie Nketiah, ambaye anaongoza safu ya mbele ya Arsenal.

Wakati huo huo, mlinda mlango Turner anakaribia kuondoka Arsenal akiwa ameichezea klabu hiyo mara Saba pekee tangu ajiunge nayo akitokea New England Revolution kwa mkataba wa thamani ya Pauni Milioni 575 msimu uliopita wa majira ya joto.

Turner mwenye umri wa miaka 29, atajiunga na Forest kwa dau la awali la Pauni Milioni Saba, ambalo linaweza kupanda hadi Pauni Milioni 10 pamoja na nyongeza.

Kuondoka kwake kunatoa nafasi kwenye kikosi kwa ajili ya kumsajili David Raya kutoka Brentford.

Klabu hizo mbili bado hazijakubaliana juu ya ada, lakini Arsenal wana uhakika wa kufikia makubaliano chini ya bei ya Brentford ya Pauni Milioni 40 na mazungumzo yanayotarajiwa kuendelea juma hili.

Chanzo: Dar24