Mon, 5 Feb 2024
Chanzo: Mwanaspoti
Wenyeji, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukayo Saka dakika ya 14, Gabriel Martinelli dakika ya 67 na Leandro Trossard dakika ya 90 na ushei, wakati bao pekee la Liverpool alijifunga Gabriel Magalhães dakika ya 45 na ushei.
Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 49 na kupanda nafasi ya pili, sasa ikizidiwa pointi mbili tu na Liverpool baada ya wote kucheza mechi 23 wakiwa mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 46 za mechi 21.
Chanzo: Mwanaspoti