Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal waichapa Liverpool, warejea kileleni mwa EPL

Gunners Arsenal.jpeg Arsenal wakishangilia moja ya magoli yao mchezo wa leo

Sun, 9 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya soka ya soka ya Arsenal imefanikiwa kuifunga klabu ya Liverpool katika dimba lake la Emirates mabao 3-2 na kufanikiwa kubeba alama zote tatu katika mchezo huo mgumu.

Arsenal ambao leo wamefanikiwa kupata ushindi wa nane katika mechi tisa walizoingia uwanjani katika ligi kuu ya England msimu huu na kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa alama 24.

Katika mchezo huo uliokua na kasi na kupokezana kwa vipindi ni washika mitutu wa London ndio walianza kupata bao kupitia kwa Gabriel Martinelli dakika ya kwanza kabisa ya mchezo kabla ya dakika ya 34 Darwin Nunez kuisawazishia Arsenal na matokeo kua moja kwa moja kabla ya mapumziko Bukayo Saka anawapa Uongozi washika mitutu na kua mabao mawili kwa moja .

Kipindi cha pili mapema kabisa dakika ya 53 Roberto Firmino anisawazishia Liverpool na mabao kua mawili kwa mawili kabla ya Thiago Alcantara kumfanyia madhambi Gabriel Jesus na kusababisha Penati ambayo Bukayo saka anafunga na kuwafanya Arsenal kushinda mabao matatu kwa mawili.arsenalKufuatia matokeo haya vijana hao wa Mikel Arteta wanaendelea kubaki kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza baada ya kufikisha alama 24 huku wakifuatiwa na Man City wenyer alama 23

Chanzo: www.tanzaniaweb.live