Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal wafunga mwaka kibabe wakiichapa Brighton

Arsenal Won 4.jpeg Arsenal wapo kileleni mwa msimamo wa EPL wakiwa na tofauti ya alama 7

Sun, 1 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vinara wa Ligi Kuu ya England, Arsenal wameuaga mwaka 2022 kwa ushindi wa ugenini wa 4-2 dhidi ya Brighton & Hove Albion jana usiku Uwanja wa The AMEX, East Sussex.

Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukayo Saka dakika ya pili, Martin Odegaard dakika ya 39, Eddie Nketiah dakika ya 47 na Gabriel Martinelli dakika ya 71, wakati ya Brighton yamefungwa na Kaoru Mitoma dakika ya 65 na kinda wa miaka 18, Evan Ferguson dakika ya 77.

Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 43 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi saba zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City, wakati Brighton inabaki na pointi zake 24 za mechi 16 nafasi ya nane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live