Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal wachezea kichapo nyumbani, Liverpool washindwe wao tu

IMG 6453.jpeg Wachezaji wa West Ham wakishangilia dhidi ya Arsenal jana usiku

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Arsenal usiku wa jana wamepunguzwa kasi katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa mabao 2-0 na West Ham United Uwanja wa Emirates Jijini London.

Mabao yaliyowazamisha The Gunners yalifungwa na Tomas Soucek dakika ya 13 na Konstantinos Mavropanos dakika ya 55 na kwa ushindi huo, Wagonga Nyundo wa London wanafikisha pointi 33 katika mchezo wa 19 na kusogea nafasi ya sita.

Kwa upande wao Arsenal baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 40 na kushukia nafasi ya pili sasa wakizidiwa pointi mbili na Liverpool kufuatia wote kucheza mechi 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live