Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal wachezea kichapo kitakatifu Emirate

IMG 4078 Arsenal Emirate.jpeg Wachezaji wa Arsenal wakiwa na masikitiko makubwa

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ndoto za Arsenal FC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England zimeyeyuka rasmi leo baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Brighton & Hove Albion FC jana Jumapili Uwanja wa Emirates Jijini London.

Mabao ya Brighton & Hove Albion yamefungwa na Julio Enciso dakika ya 51, Deniz Undav dakika ya 86 na Pervis Estupiñán dakika ya 90.

Ushindi huo unaifanya Brighton ifikishe pointi 58 katika mchezo wa 34 na kusogea nafasi ya sita, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 81 za mechi 36 nafasi ya pili.

Hii maana yake, Manchester City yenye pointi 85 za mechi 35 inahitaji kushinda mechi moja zaidi ili kutawazwa tena kuwa mabingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: