Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal wachapika ugenini Ligi ya Mabingwa Ulaya

IMG 5947.jpeg Arsenal walibubali kichapo cha magoli 2-1

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Lens wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne Uwanja wa Bollaert-Delelis mjini Lens, Ufaransa.

Mabao ya Lens yamefungwa na Adrien Thomasson dakika ya 25 na Elye Wahi dakika ya 69, wakati la Arsenal limefungwa na Gabriel Jesus dakika ya 14.

Kwa ushindi huo, Lens inafikisha pointi nne na kupanda kileleni ikiizidi pointi moja Arsenal baada ya wote kucheza mechi mbili.

Mechi nyingine ya Kundi hilo, wenyeji PSV walilazimishwa sare ya 2-2 na Sevilla ya Hispania Uwanja wa Philips mjini Eindhoven, Uholanzi.

Sevilla sasa ni ya tatu kwa pointi zake mbili, wakati PSV inaendelea kushika mkia kundini kwa pointi yake moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live