Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal vs Man City: Dakika 90 za kuamua Ubingwa EPL

FB687BD7 B016 4E2F 90AE B976BB0AD2FC.jpeg Arsenal vs Man City

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Arsenal itashuka dimbani leo kuwakaribisha klabu ya Manchester City katika dimba lao la Emirates katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza katika vita ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England.

Klabu ya Arsenal ambayo imetoka kudondosha alama katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza itakwenda kukutana na Manchester City ambayo imetoka kushinda mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Aston Villa, hivyo mchezo wa leo utakua wenye ushindani mkubwa kutokana na ubora ambao upo ndani ya vilabu hivyo.

Klabu ya Manchester City chini ya kocha Pep Guardiola imekua haipo kwenye ubora ambao umezoeleka kwa miaka kadhaa, Lakini katika mchezo wa leo dhidi ya washika bunduki wa London inaonekana kama mchezo muhimu zaidi kwa Man City kwani wakishinda mchezo wa leo watapata nafasi ya kwenda kileleni.

Klabu ya Arsenal chini ya kocha Mikel Arteta wamekua kwenye ubora mkubwa msimu huu licha ya kutopata matokeo katika michezo mitatu mfululizo mpaka sasa, Lakini mchezo wa leo utakua na umuhimu kwa klabu hiyo na kutaka kurudi kwenye njia ya ushindi.

Vita nyingine katika mchezo huu ni baina ya makocha wawili ambapo Pep Guardiola atakutana na mwanafunzi wake Mikel Arteta ambae amekua kwenye ubora mkubwa siku za karibuni, Mchezo wa leo utakua chachu ya zile mbio za ubingwa msimu huu kwa yeyote atakaeshinda mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live