Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal shughuli yao imeishia hapa UEFA

IMG 6787.jpeg Mfungaji wa bao la Bayern Munich, Joshua Kimmich

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: Tanzania

Wenyeji, Bayern Munich wamefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal ya England usiku Jumatano Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich nchini Ujerumani.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Kimataifa wa Ujerumani, Joshua Walter Kimmich dakika ya 63 akimalizia kazi nzuri ya beki Mreno, mzaliwa wa Ufaransa, Raphaƫl Guerreiro.

Bayern Munich wanatinga Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-2 kufuatia sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Aprili 9 Uwanja Emirates Jijini London.

Chanzo: Tanzania