Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal sasa ni mwendo mdundo, waichapa Chelsea

F35D0DCF 738F 497E 8933 A48F059D3E56.jpeg Wachezaji wa Arsenal wakishangilia ushindi

Sun, 6 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Arsenal imefanikiwa kuvunja daraja baada ya kuivurumisha klabu ya Chelsea wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani kwa bao moja kwa bila, ambapo washika mitutu hao wa London wakirejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Klabu ya Arsenal wamefanikiwa kupata alama tatu katika mchezo mgumu ambao ulikua unachezwa kwa tahadhari kubwa kwa pande zote mbili, Lakini vinara hao wa ligi kuu ya EPL waliweza kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

Katika mchezo huo uliokua mgumu ni beki Gabriel aliowapatia washika mitutu hao wa London bao la ushindi baada ya mpira wa kona uliopigwa na Bukayo Saka, na kuwafanya kufikisha alama 34 baada ya kucheza michezo 13 na kuwashusha klabu ya Manchester City walioongoza kwa muda.

Klabu ya Chelsea wao wanaendelea kuteremka baada ya kufungwa mchezo huo kwani wameshuka kutoka mafasi ya 6 mpaka nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Klabu ya Arsenal wao tayari wameshacheza na vigogo karibia wote kasoro klabu ya Manchester City,huku wakipoteza dhidi ya Manchester United huku wakiwa wameshinda michezo yote na kujihakikishia mazingira mazuri ya kubaki kileleni mpaka kuelekea mapumziko ya kombe la dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live