Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal pumzi imekata, walazimishwa sare Emirates

Arsenal Sare Arsenal pumzi imekata, walazimishwa sare Emirates

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Arsenal wamelazimishwa ya sare ya kufungana mabao 2-2 na Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.

Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukayo Saka kwa penalti dakika ya 70 na Eddie Nketiah dakika ya 72, wakati ya Fulham iliyomaliza pungufu baada ya beki Mnigeria, Calvin Bassey kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa mbili za njano - yamefungwa na Andreas Pereira dakika ya kwanza na Joao Palhinha dakika ya 87.

Arsenal inafikisha pointi saba katika mechi tatu za mwanzo za msimu kufuatia awali kushinda zote mbili, wakati Fulham inafikisha ponti nne baada ya awali kufungwa moja na kutoa sare moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live