Sat, 30 Oct 2021
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Baada ya kuanza Ligi kwa kusua sua mwanzoni mwa msimu, Arsenal wameimarika na wanapata matokeo kila mwisho wa wiki.
Mbao ya Gabriel Magalhães dakika ya tano na Emile Smith Rowe dakika ya 18 yameipa Arsenal ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa King Power.
Arsenal inafikisha pointi 17 na kupanda nafasi ya tano, ikiizidi pointi tatu Leicester baada ya wote kucheza mechi 10.
Matokeo hayo yanashusha presha kwa Kocha Mikel Arteta, ambaye alikua anahusishwa kufukuzwa kazi klabuni hapo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live