Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal mpaka kieleweke

IMG 4058.jpeg Arsenal mpaka kieleweke

Mon, 8 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mikel Arteta amewaambia wachezaji wa Arsenal kwamba bado wana nafasi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle na kupunguza uwiano wa pointi dhidi ya Manchester City.

Nahodha wa Arsenal, Martin Odegaard aliibuka kinara kwa kupachika bao akiisaidia timu yake kuibuka na ushindi huo mkubwa kabla ya Newcastle kujifunga kupitia mchezaji wao Fabian Schar na kuipa Arsenal bao la pili.

Baada ya ushindi huo Arsenal imekusanya ponti 82 tofauti ya pointi moja dhidi ya Man City yenye pointi 83 kwenye msimamo huku ikiwa na mechi mkononi, lakini Arteta akadai watapambana hadi mwisho.

"Ubingwa bado upo hatupo mbali sana, muhimu tunachotakiwa kufanya ni kuendeleza ushindi, kamwe tusirudi nyuma, tujiamini kila siku, tuendelea kwenda hivi hivi halafu tutaona kitachotokea, kila siku nawaambia ili upate matokeo mazuri tunatakiwa kucheza kwa kiwango bora," alisema Arteta

Arsenal ilikuwa kileleni kwa tofauti ya pointi nane kabla ya kuzingua kwenye mechi zao nne mfuulizo za mwisho na kuipa mwanya Man City kukaa kileleni.

Arsenal imebakiza michezo mitatu ambapo wikiendi itacheza dhidi ya Brighton kabla ya kumenyana na Nottingham Forest inayombana kuepuka kushuka daraja msimu huu. Washika bunduki hao wa jiji la London watacheza mechi yao ya mwisho ya msimu dhidi ya Wolves.

Wakati huo huo kiungo wa Arsenal amesifia ushindi wao dhidi ya Newcastle akidai ni hatua kubwa waliyofikia kwasasa kuelekea ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

"Tunatakiwa kuwa makini sana kipindi hiki, hatua nzuri kwetu kwa timu changa kama sisi, msimu uliopita tulipitia kipindi kigumu, kusema kweli baada ya kupoteza pointi dhidi ya Man City, kushinda dhidi ya Chelsea imeonyesha ukomavu wetu," alisema Odegaard

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: