Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal meno nje ishu ya kumsajili straika Ivan Toney

Southgate Anadokeza Kuhusu Kuanza Kwa Toney Kwenye Euro 2024 Mshambuliaji wa klabu ya Brentford Ivan Toney

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Brentford imepanga kumuuza straika wake raia wa England, Ivan Toney kwa kiasi chini ya Pauni 60 milioni katika dirisha hili jambo ambalo linaweza kuwa zuri kwa Arsenal na timu nyingine zinazomhitaji.

Inaelezwa, bei ambayo mabosi wa Brentford wameiweka kwa ajili ya kumuuza katika dirisha hili ni Pauni 80 milioni lakini kama ikitokea timu itakayokuwa tayari kulipa Pauni 60 milioni inaweza kumuuza.

Arsenal ilitaka kumsajili Toney tangu dirisha la majira ya baridi mwaka huu lakini mchezaji mwenyewe alikataa akaeleza kwamba anahitaji kumaliza msimu akiwa na Brentford ambao walimvumilia muda wote alipokuwa nje baada ya kufungiwa kwa kosa la kujuhusisha na masuala ya kubeti.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta katika ripoti yake, baada ya kumalizika kwa msimu uliopita alieleza kwamba anahitaji straika wa viwango ambaye ataenda kuongeza ubora kwenye eneo lao la ushambuliaji na miongoni mwa majina aliyoyapendekeza ni huyu Toney.

Nyota huyo alifungiwa kujihusisha na masuala ya soka kwa miezi minane baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na kubeti.

Chanzo: Mwanaspoti