Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal majanga juu ya majanga

Arsenal Ngoma Ngumu Wachezaji wa Arsenal.

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rasmi baada ya jana klabu ya Arsenal kupoteza mchezo wa robo fainali wa michuano ya UEFA dhidi ya Bayern Munich sasa wamepoteza sifa ya ushiriki wao kwenye michuano ya kombe la dunia kwa ngazi ya vilabu huku miamba ya Austria, Red Bull Salzburg wakichukua nafasi hiyo.

Kwa upande wa shirikisho la soka barani ulaya watawakilishwa na jumla ya vilabu 12 ambavyo ni Chelsea, Real Madrid, Manchester City, Bayern Munich, PSG, Inter, Porto, Benfica, Borussia Dortmund, Juventus,Salzburg na Washindi wa Ligi ya Mabingwa kwa msimu huu 2023-24.

Huku kwa upande wa Afrika(CAF) tukiwakilishwa na jumla ya vilabu 4 ambavyo ni Al Ahly, Wydad Casablanca, Washindi wa Ligi ya Mabingwa ya CAF kwa msimu huu 2023-24, na klabu nyingine itatapendekezwa na CAF kulingana na vigezo vyao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live