Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal kupitisha fagio Januari

Eddie Nketiah 1536x1063 Eddie Nketiah

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Arsenal inaripotiwa kuwa na mpango wa kuwatema wachezaji sio chini ya sita kwenye dirisha la uhamisho la mwezi Januari.

The Gunners wamajitahidi kurejea kwenye fomu kwenye wiki za hivi karibyni wakiwa chini ya Mikel Arteta na wanatarajia kufanya biashara kubwa msimu wa joto.

Kwa mujibu wa Footbal London, Alexander Lacazette na Bernd Leno ni miungoni mwa wacheza ambao Arsenal wanapanga kuachana nao, licha ya Alexander kupambana kurejea kwenye kikosi cha kwanza klabuni hapo.

Wachezaji kadhaa mikataba yao inaisha msimu ujao wa joto, na Washika bunduki wanataka kukusanya ada zao za uhamisho kabla ya kuwapoteza kama wachezaji huru msimu wa joto 2022.

Ripoti zinataja kuwa Eddie Nketia, Sead Kolasinac, Mohamed Elneny na Folarin Balogun pia wanaweza kuondoka. Wote watatu mikataba yao inaisha mwisho wa msimu, wakati mkataba wa Leno ukiisha 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live