Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal kumpa Mkataba Mpya Mikel Arteta

Mikel Arteta , Friday Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta

Wed, 23 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Arsenal inajiandaa kumpa mkataba mpya kocha wake Mikel Arteta na kumfanya kuwa miongoni mwa makocha watakao kuwa wanalipwa pesa nyingi kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Kulingana na gazeti la The Sun, Arsenal wako tayari kumpa mkataba mpya kwenye majira ya kiangazi yanayofuata baada ya kuridhishwa na kazi aliyoifanya mpaka sasa, na mradi wake wa kukijenga kikosi cha washaki bubduki wa London kuwa moja ya timu tishio.

Mkataba wake wa sasa na klabu ya Arsenal unaisha majira yajao ya kiangazi, na mkataba mpya atakaopewa anatarajiwa kuvuna kiasi cha £5million kwa mwaka, ni robo ya kiasi anacholipwa kocha wa klabu yaManchester City Pep Guardiola.

Lakini Arteta alipoulizwa kuhusu kuelezea taarifa hizo hakuwa kwenye hali ya kutaka kujibu alinukuliwa akijibu:-

“sikiliza, ni kwamba tu ni furaha hapa na kusudi langu ni kujenga klabu ambayo itakuwa na timu ya ushindi, timu ambayo watu watufarahi kuingalia, ambayo wataitambua na kuweza kubadilisha kutoka kwenye mpira tunaoutaka na kuwa kama taasisi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live