Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal kumaliza unyonge kwa Man City wikiendi hii?

Man City Vs Arsena Gg Arsenal kumaliza unyonge kwa Man City wikiendi hii?

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Arsenal anaimaliza Week end yake kwa mchezo mzito dhidi ya Manchester City, Arsenal anaenda katika mchezo huu akiwa na historia mbaya kutoka mchezo wake wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Lens walioshushiwa kichapo cha goli 2-1.

Arsenal ni kama ana bahati mbaya hivi kuelekea mchezo huu kwani nyota wake Bukayo Saka anaweza asiwe sehemu ya kikosi kitakachomkabili City week end hii kutokana na majeraha ya msuli aliyotapata katikati ya wiki hii.

Mchezo huu unanogeshwa na namna ushindani wa timu hizi mbili kwa misimu hii miwili ilivyo, msimu uliopita Arsenal aliongoza Ligi lakini dakika za mwisho City akawa Bingwa, msimu huu wameuanza kiutofauti baada ya kuchukua kombe la ngao mikononi mwa City.

Arsenal ana faida kubwa katika mchezo huu kwani anaingia akiwa hajapoteza mchezo wowote tofauti na City waliopoteza mchezo mmoja hadi hivi sasa.

Rekodi zinaonyesha kuwa katika michezo hamsini (50) iliyopita Arsenal ameshinda 17 na City ameshinda 25 na sare 8.

Katika michezo mitano (5) ya mwisho Arsenal ameshinda mchezo mmoja (1) na Man City ameshinda michezo minne (4) hakuna sare.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live