Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal kuimarisha safu yao ya Ulinzi, Arteta anamtaka huyu!

Evan Ndicka Evan Ndicka

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Arsenal wana nia ya kutaka kumnunua beki wa Eintracht Frankfurt Evan Ndicka, kwa mujibu wa ripoti.

Ndicka mwenye umri wa miaka 23, alikuwa mtu muhimu katika kikosi cha cha Frankfurt waliposhinda taji la Uropa msimu uliopita.

Beki huyo wa kati tayari amecheza mechi 16 hadi sasa kwa msimu huu, ikijumuisha mechi zote nne za Frankfurt za Ligi ya Mabingwa.

Kwa mujibu wa Evening Standard, Mikel Arteta anataka kusajili beki wa kati wa upande wa kushoto ili kushindana na mlinzi chaguo la kwanza Gabriel Magalhaes.

Ripoti hiyo inasema kuwa Arsenal walimlenga Lisandro Martinez majira ya joto, kabla ya Muargentina huyo kujiunga na Manchester United, huku pia wakimtaka Calvin Bassey aliyehamia Ajax kutoka Rangers.

Arteta ana nia ya kuongeza safu yake ya ulinzi ama Januari au msimu ujao wa joto na Ndicka atamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu. Frankfurt wanataka kuongeza mkataba wa Ndicka lakini inasemekana wanaweza kushawishika kumuuza katika dirisha la majira ya baridi ili kuepuka kumpoteza bure msimu wa joto.

Hata hivyo, Arsenal watakabiliwa na ushindani kutoka kwa vilabu kadhaa barani Ulaya ambavyo vinafuatilia hali yake, ikiwa ni pamoja na Juventus.

Arsenal wana nia ya kuimarisha upande wa kushoto wa safu yao ya ulinzi huku Gabriel chaguo lao pekee katika nafasi hiyo.

Pablo Mari, ambaye amecheza mechi 19 pekee katika michuano yote tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2020, ndiye beki pekee wa kati anayecheza upande wa kushoto, lakini yuko nje kwa mkopo katika klabu ya Monza ya Italia na anatarajiwa kuondoka kabisa mwakani.

Ndicka, ambaye alijiunga na Frankfurt akitokea AJ Auxerre mwaka 2018, ameichezea Ufaransa kuanzia chini ya umri wa miaka 16 hadi 21, lakini bado hajaifungia timu ya wakubwa.

Arsenal watarejea katika mechi ya Ligi Kuu England wikiendi hii watakaposafiri kucheza na Southampton Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live