Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal kuharakisha usajili wa kipa Garcia

Joan Garcia Joan Garcia

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi za usajili zinasema Arsenal itaharakisha juhudi zake za kumsajili golikipa wa Espanyol Joan Garcia, 23 wakati Aaron Ramsdale, 26, akitarajiwa kujiunga na Southampton kwa ada ya pauni milioni 25. (Athletic)

Mshambuliaji wa Nigeria anayecheza Napoli, Victor Osimhen, 25, ambaye ni mlengwa wa usajili wa Chelsea, amepewa ofa ya dili la miaka 4 kujiunga na klabu ya Al-Ahli ya ligi ya kulipwa Saudi Arabia lenye thamani ya pauni milioni 25 kwa mwaka. (Sky Sports)

Winga Jadon Sancho, 24, anatarajiwa kujiunga na Juventus kwa mkopo akitokea Manchester United huku kukiwa na chaguo la kumnunua. (RMC Sport)

Sancho angependa kujiunga na Chelsea badala ya Juventus na anasubiri ofa kutoka The Blues.

Aston Villa itajaribu kumsajili mshambuliaji wa Roma, Tammy Abraham, 26, iwapo mshambuliaji raia wa Colombia, Jhon Duran, 20, ataondoka klabu hiyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa.(Football Insider)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live