Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal kama jana na juzi ushindi EPL

Arsenal Vs Fulham Arsenal kama jana na juzi ushindi EPL

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Arsenal imerudisha uongozi wa pengo la pointi tano kileleni mara baada ya kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Fulham Jumapili.

Kikosi cha kocha Mikel Arteta kilibakia kileleni na alama mbili baada ya Manchester City kupata ushindi kiduchu kwa Crystal Palace lakini matokeo chanya ya Arsenal yanaifanya kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuendelea kuwa juu ya msimamo.

Mabao ya Washika Mtutu wa London yamefungwa na mlinzi wa kati wa kimataifa wa Brazil Gabriel aliyemalizia mpira wa kona wa Leandro Trossard kabla ya Gabriel Martinelli kufunga bao la pili na nahodha Martin Odegaard akaingia kambani kwa bao la tatu na kufanya The Gunners kuondoka na matokeo ya bao 3-0.

Kwenye mchezo huo, kwa mara ya kwanza ameonekana mshambuliaji Gabriel Jesus ambaye alikuwa nje ya uwanja tangia mashindano ya Kombe la Dunia alipoumia akiwa na taifa lake la Brazil.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: