Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal imedhamiria kwa Victor Osimhen

Victor Osimhen.jpeg Victor Osimhen

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: Dar24

Klabu ya Arsenal imepanga kupambana na Chelsea kuiwania saini ya Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka nchini Italia SSC Napoli, Victor Osimhen dirisha lijalo la majira ya kiangazi na miamba hiyo ya Serie A ipo tayari kumwachia.

Staa huyu wa kimataifa wa Nigeria amekuwa akiwindwa na vigogo mbalimbali Ulaya, tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini SSC Napoli ilikataa kumuuza.

Taarifa za ndani kutoka SSC Napoli zinadai timu hiyo inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 111 milioni ambayo ndio imewekwa kwenye mkataba wake.

Staa huyu mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akiwaniwa na timu nyingi kutokana na kiwango chake alichoonyesha tangu msimu uliopita.

Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2026 na tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 18 za michuano yote na kufunga mabao nane.

Mbali ya vigogo mbalimbali Ulaya kuhitaji huduma yake, saini ya fundi huyu pia inawindwa na matajiri wa Saudi Arabia.

Chanzo: Dar24