Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal hii tamu, haiachi kitu

WhatsApp Image 2024 03 13 At 11.jpeg Arsenal hii tamu, haiachi kitu

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Miaka 14 ya kutoka patupu kwenye mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, hatimaye Arsenal hii ya sasa ya kocha Mikel Arteta imevunja mwiko.

Miamba hiyo ya Emirates imepata ushindi kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora na hivyo kutinga hatua ya robo fainali baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa miaka 14. Na sasa Arsenal imeungana na vigogo wengine wa Ulaya kama Bayern Munich, Barcelona, Real Madrid, Manchester City kwa kuzitaja kwa uchache katika hatua hiyo ya nane bora.

Leandro Trossard alifunga kipindi cha kwanza kufanya ubao wa matokeo usomeke 1-1 kwenye matokeo ya jumla mbele ya FC Porto, ambao kwenye mechi ya kwanza walishinda 1-0 kwao Ureno. Baada ya dakika 120 na matokeo ya jumla kuendelea kusomeka 1-1, ilifanya mechi hiyo kuingia kwenye kupigiana mikwaju ya penalti, tukio lililotokea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya miaka minane.

Na hapo, kipa wa Arsenal, David Raya, aligeuka kuwa steringi wa mchezo baada ya kuokoa penalti mbili wa Porto zilizopigwa na Wendell na Galeno, huku kikosi hicho cha Mikel Arteta kikifunga penalti zake kupitia kwa Martin Odegaard, Kai Havertz, Bukayo Saka na Declan Rice, huku Porto waliofunga ni Pepe na Grujic kufanya penalti ziwe 4-2.

ARSENAL ILIPOKWAMA HATUA YA 16 BORA KABLA YA KUTOBOA JUMANNE

2010-11 vs Barcelona - ilichapwa 4-3

2011-12 vs AC Milan - ilichapwa 4-3

2012-13 vs Bayern Munich - sare 3-3 (ikatoka kwa bao la ugenini)

2013-14 vs Bayern Munich - ilichapwa 3-1

2014-15 vs Monaco - sare 3-3 (ikatoka kwa bao la ugenini)

2015-16 vs Barcelona - ilichapwa 5-1

2016-17 vs Bayern Munich - ilichapwa 10-2

2023-24 vs Porto - sare 1-1 (imevuka kwa penalti 4-2)

Chanzo: Mwanaspoti