Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal bwana sasa ndo nini!

Keven D Bruyne Arsenal bwana sasa ndo nini!

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Sijui tuwape pole au tuwacheke mashabiki wa Arsenal maana kwa sasa wengi presha iko juu maana matumaini ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu yameshayeyuka.

Emu tujiulize Arsenal wanapataje ubingwa mbele ya Manchester City ambayo inazidi kuwa ya moto na ina watu hasa? Ndio wanaongoza kwa pointi mbili dhidi ya Manchester City lakini wenzao wana mechi mbili mkononi ambazo wakishinda, Arsenal itapitwa kwa pointi nne.

Wale Arsenal ubingwa ulikuwa unanukia kabisa kwao, cha kushangaza wakatoka sare katika mechi tatu mfululizo hapo ndipo wakajiweka katika mazingira magumu ya kutwaa ubingwa. Katika sare zile unaweza kuwaelewa kwa ile dhidi ya Liverpool ya mabao 2-2 kwani walicheza dhidi ya timu kubwa na ngumu.

Kwa timu ambayo ina kiu ya ubingwa, ilipaswa mechi mbili zilizofuata dhidi ya Southampton na West Ham United ishinde ili kurudisha hali ya kujiamini kwa wachezaji lakini pia kuhakikisha pengo la pointi dhidi ya wanaofuata linabaki kama lilivyo.

Kama ingeshinda dhidi ya Southampton na West Ham, maana yake leo tungekuwa tunazungumzia kuwa Arsenal inaongoza kwa pointi 79 ina maana hata City ikishinda viporo vyake wangekuwa sawa.

Cha ajabu wakatoka sare nyumbani dhidi ya Southampton ya mabao 3-3 tena wakipigwa mabao mawili ya haraka ya utangulizi kipindi cha kwanza na mechi iliyofuata wakatoka sare ya mabao 2-2 na West Ham huku wakiwa wametangulia kufunga mabao mawili na walipata penalti wakakosa.

Sasa wamebaki kuomba Mungu tu Man City ipoteze mechi zake ili yenyewe itwae ubingwa wakati walikuwa na nafasi ya kutoboa bila kutegemea matokeo ya wengine.

Yaani wamekuwa kama watoto tu. Si unajua ngoma ya kitoto huwa haikeshi? Ikifika saa 12 jioni tu kila mmoja anatakiwa akalale halafu wakubwa ndio wanaingia kutamba.

Chanzo: Mwanaspoti