Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal bado tia maji tia maji, yakubali kichapo mbele ya Everton

Demarai Gray 8w251i0izwe11m40cnvunpf2f Gray akishangilia goli la dakika za lala salama

Tue, 7 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni kama homa za vipindi kwa Vijana wa Mikel Arteta, Arsenal baada ya usiku wa jana kukubali kichapo cha pili mfululizo pale Goodson Park mbele ya Everton cha magoli 2-1.

Kiwango cha Arsenal ni cha kupanda na kushuka kwani wiki chache nyuma walikua na rekodi ya kucheza michezo nane ya Ligi pasipo kupoteza.

Ila ghafla mambo yamebadilika baada ya kupokea kichapo cha magoli 4-0 kutoka kwa Liverpool, wakashinda goli 2-0 kwa New Castle kisha kati kati ya wiki iliyopita wakapoteza mbele ya United kwa magoli 3-2 na Jumatatu usiku wakapoteza tena mbele ya Everton.

Arsenal ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli katika mchezo huo likifungwa na kiungo Martin M. Oedegaard mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Kipindi cha Pili Everton walirudi kwa kasi na mipango na kujipatia magoli yaliyofungwa na Richarlison 79' kabla ya D. Gray kufunga bao la ushindi dakika za jioni 90+2

Kwa matokeo hayo Arsenal inabaki nafasi ya Saba na alama zake 23, huku Everton wakibaki nafasi ya 12 na alama zao 18.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live